Mafunzo yalifanyika Tarehe 09 Machi 2017 yalianza saa 3 Asubuhi na kumalizika saa 10 Jioni katika ukumbi wa Taasisi ta YWCA Tawi la Dar es Salaam, Buguruni Malapa.
Nini Kibaba inaweza Kufanya Mpaka sasa
Program hii itakuwezesha kutunza taarifa za Wanachama na taarifa za Fedha na michango yote ya kila siku iliwemo mikopo na Marejesho.
Kuachana na Uwakala wa Kibaba MFS
Wakala atakuwa amejiondoa mwenyewe kuwa wakala kama atafanya yafuatayo Kutofuata sheria za Nakala hii Kufanya Kosa la Jinai na Mahakama kuthibisha Malalamiko kutoka kwa Wateja na kujiridhisha ni malalamiko ya kweli Kutofikisha michango / Ada za wateja Kuamua mwenyewe kuacha Kutoza Ada zaidi ya 10% ya bei Pendekezwa
Wajibu wa Mmiliki kwa Wakala
Mmiliki atatoa msaada na sapoti kwa kipindi chote cha maisha ya Mfumo, hii itahusisha kuandaa na kusambaza machapisho, Msaada hewani (Online Support) na kuwezesha Mijadala hewani na kutoa Masasisho ya mara kwa mara (Updates).
Wajibu wa Wakala kwa Mmiliki
Wakala atawajibika kuleta taarifa zote muhimu zikiwemo (Simu, email, anuani ya Posta na Eneo) za Kikundi anacho kisajiri, hii itasaidia kuvifikia vikundi ambapo Wakala atakua ameacha uwakala.
Mmiliki wa Kibaba MFS.
Kibaba inalindwa na Haki ya Kitaifa na Kimataifa kupitia muunganiko wa Vyama vya Haki Miliki Duniani kupitia chama cha Tanzania cha COSOTA.
Wakala ni nani?
Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18+ anaweza kuwa wakala wa Kibaba VS kwa kujisali bure kwenye Tovuti ya Kibaba ambayo ni www.kibaba.co.tz