Kibaba ni Program yenye uwezo wa kurahisisha kazi zinazofanywa na Vikundi ya Kuweka na Kukopa yaani. Kibaba imetengenezwa kwa kufuata model ya ViCoBa.
Ukiwa na Programu hii utahitaji Kompyuta au simu au Tableti ili uweze kuweka kumbukumbu mbalimbali za wanachama. Hii itasaidia Kikundi kuachana na utegemezi pekee wa Kadi za Vicoba, Vitabu vya hesabu na au Excel (Spreadsheet).