Nini Kibaba inaweza Kufanya Mpaka sasa

Kibaba VS ni Program ilobuniwa ili kurahisisha kazi za kila siku za kutunza taarifa kwenye vikundi vya ViCoBa.

Program hii itakuwezesha kutunza taarifa za Wanachama na taarifa za Fedha na michango yote ya kila siku iliwemo mikopo na Marejesho.

Nini inaweza Kufanya (Kibaba Vicoba Solution Features)

 1. Kutafsiri sheria za kikundi cha ViCoBa na kuambatanisha kwenye Program
 2. Taarifa za Kikundi (Jina, Eneo, Wilaya na Mkoa)
 3. Kutengeneza na kuweka mpagilio wa Pesa kwa Kategori
 4. Kufungua Benki Akaunti na kuzitumia (Sanduku Akaunti, Akaunti Benk, Simu Pesa, Cash Akaunti)
 5. Kusajili na Kutumia Mifuko ya Jamii (Bima ya Afya, Mfuko wa Elimu, N.K)
 6. Kusajili na kuweka taarifa za Wanachama wa ViCoBa
 7. Ununuzi wa Hisa
 8. Utoaji wa Mikopo ya Hisa (Riba)
 9. Urejeshaji wa Mikopo
 10. Uchangiaji wa Mifuko ya Jamii
 11. Mikopo ya Jamii (Isiyo na Riba)
 12. Kuangalia na Kuingiza Miamala mipya (Mapato na Matumizi ya Kikundi cha ViCoBa)
 13. Muhtasari wa Kiasi kichopo (Available Balance)
 14. Mgao wa Faida (Kwa wenye ViCoBa endelevu, wanaweza kugawana faida tuu)
 15. Kujitoa kwa Mwanachama (Uwezo wa kumtoa mwanachama bila kuathili mahesabu)
 16. Adhabu (Uwezo wa kutunza kumbukumbu za fine zinazotolewa kwenye ViCoBa)
 17. Warithi (Taarifa za Warithi wako zinaweza kuingizwa kwenye mfumo)
 18. Matangazo ya Vikundi vya ViCoBa ndani ya Kibaba
 19. Uwezo wa Mwanachama asiye Admin kuona Taarifa zote za fedha pasipo yeye kubadili kitu
Forum Moderator

About The Author

Leave A Comment?

You must be logged in to post a comment.