Workshop ya mafunzo ya Kibaba MFS kwa wana ViCoBa, Singida

Workshop ya mafunzo ya Kibaba MFS kwa wana ViCoBa, Singida

Timu ya Kibaba MFS kwa kushirikiana na Mtandao wa Wilaya wa ViCoBa wa Singida, waliandaa workshop ya siku moja iliyolenga kutoa mafunzo ya awali ya jinsi ya kutumia Programu ya Kibaba MFS.

Mtandao wa Wilaya wa ViCoBa wa Singida unakuwa mtandao wa kwanza kutembelewa na timu ya Kibaba MFS, hii ikiwa ni jitihada na ufatiliaji wa karibu wa Mratibu wa Mtandao huo.

Workshop ililenga kujengea uelewa na uwezo vikundi vya ViCoBa vya Singida juu ya maswala ya matumizi ya mifumo ya elekroniki ili kuhifadhi Taarifa zao, hasa kupitia mfumo wa Kibaba MFS.

Mfumo ulipokelewa vizuri na wawakilishi wa vikundi vya VICOBA, ambapo vikundi zaidi ya 50 tayari wamesha weka order ya kuhitaji Kibaba MFS, huku washiriki wengine wakihitaji muda kwenda kuongea na wanachama wenzao ili wafanye maamuzi.

Mfumo huu wa kibaba mlio tuletea ni mzuri sana, yaani utaturahisishia sana kazi hasa mimi kama mweka hazina wa kikundi, maana tulitaabika sana kuweka kumbukumbu na taarifa za fedha wanachana wote, matumizi na mapato na mgao kwa wanachama. Kuja kwa mfumo huu utapunguza kazi na wizi uliokuwa unafanywa na baadhi ya watu wasio wema kwenye ViCoBa. Neema Kiwelu – Mweka hazina VIKWASI VICOBA GROUP

Wakati wa workshop hiyo, washiriki walipota wasaa wa kuuliza maswali na kutoa ushauri mbalimbali juu ya mfumo huu wa Kibaba, pia kulikuwa na wasaa wa majadiliano na kubadilishana uzowefu juu ya mifumo ya kielekitroniki.

Washiriki, kupitia simu janja (Smartphone) zao na Tablet, waliweza kuingia kwenye demo ya mfumo wa Kibaba, (Bonyeza hapa ili kutumia mfumo ) na kwenda sambamba na mwezeshaji. Njia hii iliwafanya wote kushiriki kwa pamoja.

Kutoka Timu ya Kibaba MFS walishiriki

  1. Frank Mwasalukwa – Project Lead Developer.
  2. Rogers Fungo – Project Coordinator / Lobbyist.

Picha na Matukio mbalimbali.

Forum Moderator

About The Author

Leave A Comment?

You must be logged in to post a comment.