Programu ya Kibaba MFS itamnufaishaje mwanachama wa VICOBA ?

Programu ya Kibaba MFS itamnufaishaje mwanachama wa VICOBA ?

Kwanini VICOBA

Siri moja wapo ya kuwa tajiri ni kujenga tabia ya kuweka akiba. Kwa wajasiriamali wadogo swala la kuweka pesa zao benki na kukopa huwa ni swala gumu hasa vijijini ambako hakuna huduma hiyo, kuna njia nyingine ambayo wataalamu wamebuni kuwawezesha kuitumia nayo ni  kuweka akiba zao kwenye VICOBA (Village Community Banks )

Utunzaji wa Taarifa za VICOBA

Vikundi vya VICOBA vimeundwa kutumia utaratibu wa kuweka kumbukumbu zao kwenye Kadi / karatasi zilizochapwa ki mfumo na utaratibu wa VICOBA ili kutunza taarifa za ununuzi wa Hisa, michango ya mfuko wa Jamii na Mikopo yote. Taarifa hizi huwekwa kwenye Sanduku (Safe) pamoja na fedha za michango ya wanachama.

Changamoto ya Utunzaji na ukokotoaji wa taarifa za Kifedha

Vikundi vingi vya VICOBA vimekuwa maeneo ya Vijijini ambapo matukio kama ya mafuriko, usalama wa taarifa za kwenye kadi, unyevu unaopelekea taarifa kufutika au kupotea kabisa. Hii imesababisha hasara na ugomvi kwa baina ya wanachama wa VICOBA.

Ukokotoaji wa mikopo na mgao wa faida kwa mwaka hufanyika kulingana na Hisa za mwanachama dhidi ya kipato kilichotokana na miradi au mikopo ya kikundi. Changamoto kubwa hutokea baada ya mwaka mzima wa mapato na matumizi na ukokotowo wa mahesabu ya mgao wa faida na kupelekea baadhi ya wanachama kupata zaidi au wengine kupata wasicho stahiri.

Suluhisho kwa Kutumia Kibaba VS

Kibaba ni Program yenye uwezo wa kurahisisha kazi zinazofanywa na Vikundi ya Kuweka na Kukopa yaani ViCoBa na vukundi vya aina hiyo.

Ukiwa na Programu hii utahitaji Kompyuta au simu au Tableti ili uweze kuweka kumbukumbu mbalimbali za wanachama. Hii itasaidia Kikundi kuachana na utegemezi pekee wa Kadi, Vitabu vya hesabu na Excel (Spreadsheet).

Ukiwa na Programu hii itakufanya uwe na maisha yasiyo na MSONGO kwa kuwa kazi kubwa pekee mbele yako itakua ni Kuingiza data kwenye mfumo huu wa Kibaba MFS, ukokotoaji uliobaki utafanywa na Programu yenyewe.

Jinsi Mfumo unavyofanya Kazi

Kibaba ni Programu iliyotengenezwa ili kufanya kazi kwenye Wavuti (Web-based Application), mfumo unafanya kazi kwenye vifaa tofauti tofauti ili mradi tuu ina Browser na Intaneti.

Kikundi kikinunua programu hii, kitapewa anuani yake ambayo ataitumia kuingia na kufanya maingizo yake. mfano wa anuani utakuwa jinalakikundi.kibaba.co.tz . Taarifa zote za kikundi zitahifadhiwa ndani ya database iliyo chini ya mfumo wa mradi wa Kibaba. Taarifa hizi hukaa kwenye SEVA za kampuni ya Microsoft kupitia mradi wake wa mawinguni (Cloud Base) ujulikanao kama Microsoft Azure. Kazi ya mtumiaji ni kuingiza Data, kazi ya Kibaba MFS ni kuunganisha na kutoa msaada, wakati Microsoft Azure inatuhakikishia usalama wa taarifa zetu.

Jinsi Usalama wa Taarifa zako unavyofanya kazi

Forum Moderator

About The Author

Leave A Comment?

You must be logged in to post a comment.