Timu ya Kibaba imeendesha mafunzo ya jinsi ya kuandaa na kutumia mfumo wa Kibaba kwa wanachama viongozi wa Vikundi vya ViCoBa , safari hii ilishirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya “Young Women Christian Association” kama inavyojulikana zaidi kwa jina la YWCA.
Mafunzo hayo yaliwalenga wanachama viongozi wa Vikundi vya VICOBA vilivyonunua mfumo wa Kibaba kwa wilaya ya Ilala, Dar es Salaam ambavyo vinasimamiwa na taasisi ya YWCA Tanzania. Mafunzo yalilenga kuwapa uwezo wa uelewa wa jinsi mfumo mzima wa Kibaba unavyofanya kazi, yaani kuanzia utaarishaji wa mfumo, mahali data zao zitahifadhiwa, jinsi mfumo unavyofanya kazi na matumizi yake kwa ujumla.
Frank Mwasalukwa, ambaye ni kiongozi wa Mradi wa Kibaba, alianza kwa kutoa utambulisho wa mfumo na wapi wazo la kutengeneza Mfumo wa Kibaba ulipotokea,
Tuliamua kutengeneza mfumo huu ili kukidhi haja ya uhitaji wa utunzaji wa taarifa za kikundi chetu binafsi cha ViCoBa – Alisema Mwasalukwa
Aliendelea kuwaeleza washiriki juu ya Mfumo wa Kibaba unavyoshirikiana na mifumo mingine duniani ili kufikisha huduma kwa uhakika na upatikanaji wa huduma hewani kwa asilimia 99.9% bila kukatika, Kibaba VS inashirikiana na mfumo wa Microsoft Azure kuhifadhi taarifa za wanachama wa ViCoBa wanaotumia mfumo wa Kibaba. Microsoft Azure imethibitishwa kuwa yenye Ufanisi wa hali ya juu na ya Kuaminika.
Rogers B. Fungo, Mshawishi na Mratibu wa Mafunzo wa Mfumo wa Kibaba kwa vikundi vya ViCoBa, aliwezesha washiriki wa mafunzo hayo kufanya kwa vitendo kazi ya kuandaa na kuutumia mfumo wa Kibaba, Bw. Fungo aliweza kufananisha mfumo mzima wa ViCoBa na mfumo mzima wa Kibaba ili washiriki waelewe mfumo kirahisi. Baadae washiriki walitengwa kwenye makundi kulingana na vikundi wanavyowakisha ili kuweza kuingiza taarifa.
Kwa ujumla washiriki walifurahia mafunzo, na kuahidi kuwasumbua wawezeshaji pale watakapopata shida wakati wa matumizi. Wawezeshaji walitoa Namba za simu zitumikazo wakati wowote, barua pepe na Tovuti ya kibaba ambayo ni kama Portal ya Mfumo wa Kibaba.
Mafunzo yalifanyika Tarehe 09 Machi 2017 yalianza saa 3 Asubuhi na kumalizika saa 10 Jioni katika ukumbi wa Taasisi ta YWCA Tawi la Dar es Salaam, Buguruni Malapa.
Kutoka Kibaba MFS
- Frank Mwasalukwa – Kiongozi Mradi wa Kibaba MFS
- Rogers Fungo – Mashawishi / Mtaalam wa Elimu ya Kibaba MFS
Kutoka Young Women Christian Association – YWCA
- Rose Manumba – Lawyer and Program Coordinator (Enabling Economic Empowerment and Justice to Women/Young Women)
Leave A Comment?
You must be logged in to post a comment.