Wanakikundi wa kikundi cha kuweka na kukopa maalufu kama VICOBA kijulikanacho kwa jina la Mwijangasyege kilichopo kata ya Isange wilayani Rungwe mkoani Mbeya , wameingia kwenye hali ya sintofahamu baada ya pesa zao kukwapuliwa na kuku kwa njiia ya kishirikina.
Wakiongea na kituo hiki kwa masikitiko makubwa , walisema tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati wa mahesabu ya fedha hizo, ambapo kufumba na kufumbua alitokea kuku mweupe na kudonoa fedha kiasi cha shilingi laki nne na thelathini na kisha kutokomea kusikojulikana.
Hamu kitaje mmoja wa wanakikundi , alisema wanashindwa kuelewa juu ya kilichokuwa nyuma ya kuku huyo ambaye alifika eneo la tukio kama mwewe na kukwapua pesa na kisha kutokomea nazo.
‘’Ilikuwa hali ya taharuki, majira ya saa kumi na moja jioni wakati tukiwa katika mahesabu ya fedha ambazo tulitaka kugawana lakini wakati tukiendelea na zoezi hilo kufumba na kufumbua alitokea kuku rangi nyeupe huku akiwa anarukaruka mithili ya mwewe akafika eneo la tukio na kutua pembeni huku akituangalia na kukodolea macho bulungutu la pesa, ambapo baada ya kumaliza kazi ya kuhesabu fedha zote tukaziweka kwenye ungo nandipo ghafla kukatokea hali kama ukungu hali iliyotufanya tusijue kinachoendelea na sekunde chache baadaye kupigwa butwaa baada ya kuona pesa hazipo ’’ Alisema kitaje.
Akifafanua kuhusu tukio hilo, Katibu wa kikundi hicho ,Basimenye silimmani ,alisema jumla ya pesa ilikuwa milioni mbili laki nne na tisini elfu, ambapo kati ya pesa hiyo, shilingi laki nne na thelathini ndizo zilizo kwapuliwa na kuku huyo na kupelekea sintofahamu miongoni mwao .
Aidha katibu huyo allisema mpaka sasa hawaelewi cha kufanya na badala yake wanaendelea kusuburi kitakachojili kwani wanamtegemea mungu kama ndie muweza wa yote,
‘’kama wanakikundi hatujaenda kokote kwa ajili ya kupata uvumbuzi na kujua kulikoni kuhusiana na kuku huyo na hivyo tunamwachia mungu mwenyewe’’ alisema silimmani.
Leave A Comment?
You must be logged in to post a comment.