Forum Navigation
You need to log in to create posts and topics.

Jinsi ya kufuta kikundi kwenye Kibaba

Watu wengi wamekuwa wakiuliza jinsi ya kufuta kundi kwenye Kibaba.

Ili kufuta kikundi kabisa
Hatua za kufata
1. Tuma namba yako ya usajili au uthibitisho uliyoipata wakati unajisajili.
2. Tuma namba ya ufunguo ya umma ya kikundi
3. Eleza sababu za kufunga.
4. Ndani ya saa 24 sms zitatumwa kwa wanachama wote wa kikundi chako, kuwa unataka kufuta kikundi.

NB:
1. Jinsi ya kupata namba yako ya usajili,
a). Kwenye PC - nenda alama ya picha juu upande wa kulia, kisha bonyeza wasifu wangu, utapata namba yako

b). Kwa app na simu ya mkononi, nenda kwenye mipangilio, kisha wasifu wangu, hapo utapata namba ya yako.

2. Jinsi ya kupata namba ya group.
a). Kwa PC, nenda kwenye menyu ya mipangilio, kisha nenda kwenye Taarifa za kikundi, hapo utapata ufunguo wa umma
b). Ingia kama admin, kisha nenda kwenye mipangilio, kisha bonyeza namba ya utambulisho.

Uploaded files:
  • Screen-Shot-2020-12-10-at-10.45.11.png
  • Screen-Shot-2020-12-10-at-10.47.31.png