Vicoba ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mfumo wa uendeshaji wa kikundi cha ViCoBa hutofautiana katika sheria na utaratibu kulingana na matakwa ya wanachama. Kikundi cha ViCoBa kinakuwa na Wanachama wasiozidi 30, Kikundi kinajiwekea utaratibu wa siku ya kukutana kwa nafasi zao, pia kikundi huweka kiasi cha thamani ya Hisa moja na idadi ya hisa zisizozidi 5 kwa mwanachama ambazo zita nunuliwa mara moja kila wakutanapo.
Kikundi kinaweza kuweka utaratibu wa michango kadri wanavyoona inafaa kwa ajiri ya maendeleo ya Kikundi na wao wenyewe Binafsi. Kwa mfano kikundi kinaweza kuweka kiasi cha adhabu kwa wachelewaji kikaoni au adhabu kwa wasiohuhuria vikao, wanaweza kuongeza mifuko mingine ya Jamii kadri wanavyo hitaji.
Ki msingi, Mfumo wa ViCoBa hutumia Kadi/Vitabu vya kurekodi Hisa na Mapato ya Kikundi/ wanachama na Sanduku hutumika kama kifaa cha kuhifadhia Pesa na nyaraka mbalimbali za Kikundi zikiwemo kadi za kutunza Taarifa.
kulingani na ukuaji wa vikundi vya ViCoBa na changamoto za utunzaji wa Fedha na Taarifa zake umekuwa ni shida sana, wakati mwingine, taarifa za wanachama hupotea kuokana na sababu mbalimbali kama majanga yasiyotarajiwa ya Wizi, Mafuriko na mengineyo. Vikundi vikiwa na pesa za nyingi huamua kufungua akaunti ya Fedha benki au kwenye akaunti za simu za mkononi, lakini Taarifa za wanachama hubaki kutokuwa salama kwa kutotunzwa vizuri.
Kibaba VS ni mfumo wa kurahisisha kazi za ViCoBa ili kuleta ufanisi kwenye utunzaji wa Taarifa binafsi za wanachama na taarifa za Fedha. Kwa kutumia kibaba utaweza kuepukana na ujazaji wa taarifa zako kwenye Vitabu na kadi zisizo salama au matumizi ya Spreadsheet (Excel).
Mfumo wa Kibaba VS, humuezesha mweka hazina wa kikundi kupata taarifa za fedha za mwanachama yeyote, wakati wowote kwa kutumia kifaa chenye uwezo wa wavuti (Internet). Vifaa kama Simu Janja (Smart Phone ), Tablet na Computer vikiwa na internet basi atapata huduma hiyo.
Leave A Comment?
You must be logged in to post a comment.