Mmiliki na mwenye haki zote juu wa Mfumo wa Kibaba MFS ni Kampuni inayojishughulisha na maswala ya IT na utengenezaji mifumo ya Kompyuta ya Luton Consult. Kampuni hii ina haki zote juu ya mfumo huu na inahifadhi haki ya Kukubali au kukataa Mtu binafsi, Chama, Kikundi, kampuni au hata Taasisi yeyote ya (Kiserikali na isiyo ya Kiserikali) kununua na kumiliki mfumo wa Kibaba VS.
Kibaba VS imesajiriwa na chama cha Haki miliki cha Tanzania (COSOTA) nembo na majina yanayotumika (Kibaba VS, Kibaba MFS na Kibaba Haba na Haba) yana utambulisho wa kutumika kama alama za Biashara (Trade Mark au TM) kutoka kwa Wakala wa Serikali wa Usajiri na utoaji Leseni (BRELA).
Kibaba inalindwa na Haki ya Kitaifa na Kimataifa kupitia muunganiko wa Vyama vya Haki Miliki Duniani kupitia chama cha Tanzania cha COSOTA.