Jinsi ya kutunga Sheria za Kikundi

Sheria za kikundi hutungwa na Kikundi na ndio ambazo huongoza kikundi cha Vicoba. Kibaba VS imeweka utaratibu wa kuchukua sharia mbalimbali za kikundi husika ili uweze kutumia Programu hii kwa ufasaha kama kundi.

Ili kuweka sheria za kikundi.
1. Nenda kwenye menyu ya Mipangilio
2. Bonyeza Sheria
3. Jaza Sheria za Kikundi chako kama mlivyokubaliana

1. Taratibu za Michango

Ada ya Kujiunga

Hii ni Ada ambayo mwanachama analipa kwenye kikundi chake ili aweze kuwa mwanachama. Si kila kikundi kina ada ya kujiunga, na kama hakuna ada ya kujiunga basi jaza Sufuri (0)

Kima cha chini ya Michango/Hisa

Tunajia kila kikundi kina kima cha chini cha uchangiaji au ununuzi wa Hisa. Hapa utaingiza kiasi chini cha gharama ya Hisa, yaani kama thamani ya hisa 5 ni 25,000 basi kima cha chini ni 5,000 ambayo ni sawa na Hisa moja.

Kima cha chini Michango ya Jamii

Vikundi vingi vya Vicoba huwa na Mfuko wa Jamii, hapa utaweka kiasi mchokubaliana kuchangia kila mnapokutana.

2.Taratibu za Mikopo

Muda wa Mkopo

Huu ni muda unaotakiwa kupita kabla ya mwanachama hajawa na uwezo wa kukopa. Mfano:kwa mwanachama mpya anatakiwa akae miezi mitatu huku akiwa anachangia ndipo aweze kukopa

Michango kabla ya Mkopo

Rahisi tuu, Je mwanachama mpya anatakiwa awe ameshachangia au amenunua HISA mara n gapi ili aweze kukopeshwa?

Muda wa Mkopo

Huu ndio muda ambao utatumika kuhesabu miezi ya mkopo au tarehe ya mwisho ya marejecho ya mkopo.

Riba

Katika asilimia, hiki ni kima ambacho ninatumika kama ziada atakayolipa mwanachama endapo atakopa.

Makato ya Bima

Kwa mwanachama atakaechukua mkopo kama kuna makato ya Bima ya Mkopo basi yanawekwa hapa katika asilimia.

Malipo yaliyochelewa

Hii ni adhabu anayopewa mkopaji kwa kuchelewa kulipa marejesho yake.

3.Gawio

Andaa Mfumo kwa ajiri ya Gawio

Sehemu hii ni maalum pale tu kundi linapokuwa kwenye mchakato wa kugawana mali za Kikundi. Usichague kama huwaja tayari kuingia kipengele cha kugawana.

Mwanachama anachukua Hisa pekee

Chaguo hili ni kama mgao wa kikundi unaenda kugawana Hisa Pekee, yaani kwenye kufunga kikundi kama wanakikundi wanataka kuchukua Hisa zao pekee na kuacha faida.

Mwanachama anachuka faida pekee

Kama makubaliano ni tofauti hayo ya juu, Manakikundi wanaweka kukubaliana kuchukua Faida Pekee na kuacha Hisa zao.

Anachukua Pesa yote (Faida + Hisa)

Kama kikundi kimeamua kila mwanachama anachukua pesa yake na kuanza upya.

4.Mengineyo

Kiasi cha Kujitoa

Kwa mwanachama anayejitoa, kama kunamakato ya kujitoa basi unayaweka kwa asilimia. Hii itakokotoa kiasi atakachobakiza kundini endapo ataamua kujitoa.

Akaunti ya Benki

Hapa chagua akaunti itakayotumika kama ya kwanza (default). Miamala yote itakuwa inainza pesa huku.

Muundo wa Uchangiaji

Chagua muundo wa uchangiaji wa Kikundi chako.

Was this article helpful?

Related Articles