Uwakala wa Kibaba MFS (Mwongozo)

Wakala ni nani ?

Mwongozo huu unamuhusu Mtu yeyote wa pili asiye mfanyakazi au mshauri (consultant) wa Bibo Solutions Ltd na kampuni zake dada  za (Kibaba MFS na Smart Labs).

Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18+ anaweza kuwa wakala wa Kibaba MFS kwa kujisali bure kwenye Tovuti ya Kibaba ambayo ni www.kibaba.co.tz kisha kuweza kusajiri vikundi mbalimbali vya ViCoBa na vingine vya aina hiyo vyenye uhitaji wa kutumia mfumo huu wa Kibaba MFS.

Mmiliki wa Kibaba MFS (Bibo Solutions ltd.)

Mmiliki na mwenye haki zote juu wa Mfumo wa Kibaba MFS ni Kampuni inayojishughulisha na maswala ya IT na utengenezaji mifumo ya Kompyuta ya Bibo Solutions Ltd. Kampuni hii ina haki zote juu ya mfumo huu na inahifadhi haki ya Kukubali au kukataa Mtu binafsi, Chama, Kikundi, kampuni au hata Taasisi yeyote ya (Kiserikali na isiyo ya Kiserikali) kununua na kumiliki mfumo wa Kibaba MFS.

Kibaba MFS imesajiriwa na chama cha Haki miliki cha Tanzania (COSOTA) nembo na majina yanayotumika (Kibaba, Kibaba MFS na Kibaba Haba na Haba) yana utambulisho wa kutumika kama alama za Biashara (Trade Mark au TM) kutoka kwa Wakala wa Serikali wa Usajiri na utoaji Leseni (BRELA).

Kibaba inalindwa na Haki ya Kitaifa na Kimataifa kupitia muunganiko wa Vyama vya Haki Miliki Duniani kupitia chama cha Tanzania cha COSOTA.

Wajibu wa Wakala kwa Mmiliki

Wakala atawajibika kuwasilisha malipo yote ya Mteja kwenye Ofisi za Kibaba MFS au Bibo Solutions Ltd au Mpesa/tiGO Pesa au Benki kabla huduma haijaanza kutolewa. Wakala hato ruhusiwa kutoza zaidi ya 10% ya bei pendekezwa, hii aihuishi Mapatato ya Wakala na Wateja wake juu ya Mafunzo ya matumizi ya Kibaba MFS.

Wakala atawajibika kuleta taarifa zote muhimu zikiwemo (Simu, email, anuani ya Posta na Eneo) za Kikundi anacho kisajiri, hii itasaidia kuvifikia vikundi ambapo Wakala atakua ameacha uwakala.

Wajibu wa Mmiliki kwa Wakala

Mmiliki wa Kibaba MFS anawajibika kutoa mafunzo na matirio (Machapisho) ya Kibaba MFS kwa Wakala alisajiliwa kwa wakati ili kumwezesha Wakala kuwahudumia wateja wake. Wakala atapata 10% ya Mauzo ya Kibaba MFS, pesa hii itakusanywa na malipo kufanyika kwenye Akounti ya wakala (Benki au Simu).

Mmiliki anawajibika kutoa huduma ya kuwepo kwa mfumo wa Kibaba MFS hewani (Online) kwa masaa 24 ndani ya wiki na mwaka (24/7365) ndani ya kipindi ambacho mteja atakuwa amelipia huduma.

Mmiliki atatoa msaada na sapoti kwa kipindi chote cha maisha ya Mfumo, hii itahusisha kuandaa na kusambaza machapisho, Msaada hewani (Online Support) na kuwezesha Mijadala hewani na kutoa Masasisho ya mara kwa mara (Updates).

Kuachana na Uwakala wa Kibaba MFS

Wakala atakuwa amejiondoa mwenyewe kuwa wakala kama atafanya yafuatayo

  1. Kutofuata sheria za Nakala hii
  2. Kufanya Kosa la Jinai na Mahakama kuthibisha
  3. Malalamiko kutoka kwa Wateja na kujiridhisha ni malalamiko ya kweli
  4. Kutofikisha michango / Ada za wateja
  5. Kuamua mwenyewe kuacha
  6. Kutoza Ada zaidi ya 10% ya bei Pendekezwa

Kujiunga kuwa Wakala

Kwa yeyote anaetaka kuwa wakala atajaza fomu kwenye Tovuti hii na Timu ya kibaba itamthibitisha kwa kukubali au kukataa kwa yeye kuwa Wakala wa Kibaba MFS.

Kwa yeyote atakaekuwa amejitoa uwakala, atatakiwa kijiunga tena kwa kujaza fomu upya ili kuwa wakala.

Mawakala wote watachapishwa kwenye Tovuti hii pindi tu watakapopitishwa na Timu ya Kibaba MFS.