Kuhusu Kibaba MFS

Kibaba ni Program yenye uwezo wa kurahisisha kazi zinazofanywa na Vikundi ya Kuweka na Kukopa yaani ViCoBa, MFI na Upatu.

Ukiwa na Programu hii utahitaji Kompyuta au simu au Tableti ili uweze kuweka kumbukumbu mbalimbali za wanachama. Hii itasaidia Kikundi kuachana na utegemezi pekee wa Kadi, Vitabu vya hesabu na Excel (Spreadsheet).

Boresha Kwa Matumizi yako

Kibaba unaweza kuiboresha (Customisation)ili kuendana na Sheria za kikundi chako cha ViCoBa.

Hifadhi Taarifa za Wanachama

Kibaba inakuwezesha kuhifadhi taarifa za wanachama wako, Taarifa bifsi za wanachama zitakazowezesha kumtambua wakati wowote

Taarifa za Hisa na Mikopo

Weka kumbukumbu za Hisa za wanachama wako pamoja na Taarifa za Mikopo, Mfuko wa Jamii na Mgao wa mwaka.

Vipengele kwenye Kibaba MFS (Features)

Vipengele vinavyounda Mfumo wakibaba MFS.
 • Wanachama

  Kibaba inakuwezesha kuhifadhi taarifa za wanachama wako, Taarifa bifsi za wanachama zitakazowezesha kumtambua wakati wowote.

 • Mfuko wa Jamii

  Mfumo utakuwezesha kuandikisha Mifuko mbalimbali ya Jamii, kama Bima ya Afya, Elimu na mingineyo

 • Mikopo Hisa / Jamii

  Rekodi mikopo yote ya Wanachama, pata kumbukumbu ya kuchukuliwa mkopo na Tarehe ya Kurudisha mkopo

 • Miamala ya Kifedha (Transactions)

  Tunza kumbukumbu zote za Mapato na Matumizi kupitia kipengele hiki cha Miamala, hapa utaweza kurekodi tarifa za fedha.

 • Hamisho la Fedha

  Unaweza kufanya hamisho la Fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine. Kama vile simu pesa kwenda Akounti yenu ya Benki

 • Matangazo

  Mfumo unawezesha wanachama kuweka nakusambaza Matangazo / Ujumbe kwenye mtandao wa Kibaba, na wanachama wote wakaona.

 • Urithi / Inheritance

  Mfumo unaruhusu kuhifadhi taarifa za Warithi wa Mwanachama, unaweza kuweka hadi warithi 5 kwenye Databezi

 • Ununuzi wa Hisa

  Tunza taarifa na kumbukumbu za ununuaji wa Hisa za wanachama wa kikundi chako. Taafizi hizi hutumika kwnye mgao wa Mapato

 • Michango Maalum

  Unaweza kuanzisha na kukusanya Pesa kwa kutumia mfuko maalum, kuchangia mambo kama msiba, sherehe na N.K

 • Marejesho ya Mkopo Hisa / Jamii

  Rekodi marejesho ya mikopo ya Wanachama, Tarehe na Kiasi. Mpaka mkopo uishapo, na mfumo kukujilisha.

 • Akaunti za Fedha

  Unaweza kufungua Akaunti za fedha na kumbukumbu zake, inaweza kuwa Sanduku, Simu au hata Akaunti ya Benki.

 • Mgao (Dividend)

  Mfumo huu utakusaidia kufanya hesabu za mgao wa pesa, hesabu hufanyika kutokana na  ununuzi wa hisa.

 • Upigaji Kura

  Ukitumiamfumo wa Kibaba, kufanya maamuzi ya pamoja ni rahisi, mfumo unaruhusu wanachama kuanzisha na kupigia kura jambo fulani.

 • Kujitoa Uanachama

  Mfumo unaruhusu kujitoa kwa Mwanachama, Taarifa zake zitabaki, ila Akaunti yake itakua sufuri.

Timu ya Kibaba MFS (The Owesome team)

Timu hii ya Maajabu, iko tayari kukusaidia wakati wowote ukipata swali / tatizo / maoni. Karibu sana.
Founder / Kibaba MFS Project Lead

Frank, mmoja ya walionzaisha Kibaba MFS, ana uzowefu usiopungua miaka 10 kwenye maswala ya Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ameshiriki kwenye Miradi mbalimbali ya TEHAMA na amekuwa Mkurugenzi wa Kiufundi wa kampuni mama ya Bibo Solutions.

Frank R. Mwasalukwa

Founder / Project Lead

null

Lilian, Mtaalam wa TEHAMA na Uongozi, amekua mstari wa mbele kuhakikisha ubora na umakini wa hali ya Juu kwenye utengenezaji wa Mifumo. Ana stashahada ya Mifumo ya Kompyuta kutoka chuo kikuu cha Greenwich.

Lilian W. Mushi

Founder / Project Finance
null

Rogers, amefanya kazi ya kuelimisha watu mbalimbali, wazee na vijana juu ya maswala ya Maadili na Uepukaji wa Migogoro na kutafuta Amani, amefanya kazi ya kuzunguka Tanzania nzima kuanzisha na kuunganisha vikundi vya ViCoBa katika wilaya. Mtaalamu wa Elimu ya ViCoBa

Rogers B. Fungo

Project Cordinator / Lobbyist
Rose Monyo, Customer Care / Sales

Rose, mwajiriwa wa Bibo Solutions kama Sales Executive, amekua mtu muhimu kwenye uuzaji wa bidhaa mbalimbali za Bibo. Sasa pia anahudumu kama HUDUMA kwa Wateja wa Kibaba.

Rose H. Monyo

Customer Care / Sales